Ngorongoro Heroes Yatupwa Nje Kuelekea AFCON U20 Yapigwa Na Mali Nje Ndani.
Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 'Ngorongoro heroes' imetolewa katika michuano ya Afrika kwa kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Mali.
Ngorongoro inayonolewa na kocha Ammy Ninje imetolewa kwa jumla ya mabao 6-2 kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika hapa nchini.
Vijana hao ambao wengi wao wametoka kwenye kikosi cha timu ya vijana chini miaka 17 'Serengeti Boys' kilichoshiriki michuano ya Afrika mwaka jana kilionekana kushindwa kufua dafu mbele ya wenyeji hao.
Mabao ya Mali yalifungwa na Hajji Dubey dakika ya 39 kabla ya Diadie Dianka kufunga la pili kwa mkwaju wa penati dakika kumi baadae.
Samake aliifungia Mali mabao mawili dakika ya 63 na 66 wakati bao la kufuatia machozi la Ngorongoro lilifungwa na Habib Kiyombo dakika ya 61

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.