Kocha Yanga Aiongoza DR Congo Kupata Sare Dhidi Ya Nigeria.


Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera jana alikuwepo kwenye benchi la ufundi la DR Congo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Zahera anatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam wakati wowote kuungana na kikosi cha Yanga kinachokwenda Kenya kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano/usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema wanazo fedha za kutosha kufanya usajili wa 'nguvu' lakini wanamsubiri kocha huyo kwa kuwa yeye ndiye bosi wa zoezi zima.

Baada ya 'kumkata' Ngoma, Zahera anasubiriwa kufanya maamuzi juu ya wachezaji wengine anaotaka kubaki nao msimu ujao kwenye kikosi cha Yanga.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.