Hii Hapa Taarifa Kamili Kuhisi Usajili WA Ngassa Yanga.


Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha taarifa zilizoenea mitandaoni zikidai kuwa wameanza mazungumzo na mchezaji wake wa zamani, Mrisho Khalfan Ngassa, ili kumrejesha.

Mkuu wa Kamati ya Kamati ya Usajili na Maadili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, ameeleza kuwa hakuna ukweli juu ya hilo na badala yake mchezaji huyo aliwasili katika makao makuu ya klabu hiyo kusalimia.

Nyika ameeleza kuwa Ngassa aliwasili kuwapa salaam na si kusajiliwa kama ambavyo taarifa nyingi zimekuwa zikieleza.

Ngassa ambaye aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa katika ligi, alijiunga na Mbeya City FC kisha kutimkia Ndanda FC ya Mtwara iliyoepuka kushuka daraja mwishoni mwa msimu.

Wakati huo Yanga kesho inaondoka kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Juni 3 2018 jijini Nairobi.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.