SIMBA WABADILI GIA ANGANI SASA KUIPIKU YANGA KWA DJAKO.



-Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba imebadili gia angani na kutoka Zambia hadi Togo kupitia Ethiopia. Baada ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Christopher Katongo ambaye anaichezea klabu ya Green Buffaloes ya Zambia na Sasa wameamua kusubili kwanza kufanya usajili wa mkongwe huyo.

-Unajua kwa nini wamepiga pozi kwanza kwa  Katongo ambaye alitajwa na kocha wa kikosi cha Simba, Pierre Lechantre kusajiliwa na klabu ya Simba ila baada ya kuona mkataba wa mshambuliaji wa Togo, Arafat Djako umeisha na klabu ya yake ya Welayta Dicha ya Ethiopia ndio Simba wakabadili gia angani.

-Sasa Simba wanamtaka kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Togo na kuachana na mshambuliaji Christopher Katongo mwenye umri wa miaka 35 kutokana na kuwa na umri mkubwa na pia ana mkataba na klabu ya Green Buffaloes ya Zambia.

-Mshambuliaji huyo alikuwa ameshafanya mazungumzo na klabu ya Yanga na kila kitu walikuwa wameshakubaliana ila alikuwa anasubiliwa kocha mpya wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera apitishe usajili huo ili kamati ya usajili iweze kumsajili ila mpaka sasa hamna chochote kinachoendele.

@yossima Sitta Jr.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.