Mshambuliaji Majimaji Fc Awakaba Koo Chirwa Na Bocco



Mshambuliji Marcel Bonaventure 'Kaheza' amewapa presha washambuliaji Obrey Chirwa nae John Bocco baada ya kufunga mabao matatu 'hat trick' kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

Kaheza amefikisha mabao 13 akimzidi Chirwa bao moja na kuzidiwa moja pia na Bocco aliye nafasi ya pili.

Mshambuliji Emmanuel Okwi wa Simba ndiye kinara wa ufungaji kwa sasa akiwa amepachika mabao 19 mpaka sasa.

Licha ya Majimaji kuwa kwenye kipindi kigumu kwenye msimamo ikiwa nafasi ya tatu kutoka chini lakini Kaheza ameendelea kufunga mabao kila anapopata nafasi.

Mabao hayo ya Kaheza yameitoa Majimaji mkiani mwa msimamo wa ligi nakupanda nafasi mbili.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.