Yanga Kufanya Mkutano Mkuu Mwezi Mei
Kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga kilichofanyika Jumapili iliyopita, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ametangaza tarehe ya kufanyika Mkutano Mkuu wa Wanachama.
Mkwasa amesema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 05 May 2018.
Ajenda za Mkutano huo zitawekwa hadharani baadae.
Mkwasa amewataka Wanachama wote kuhakikisha wamelipia ada zao za mwaka ili wasikose fursa ya kushiriki Mkutano huo.
Yanga imekuwa katika mchakato wa kufanya mabadiliko, bila shaka Mkutano huo ni mwanzo wa mafanikio ya mchakato huo ambao umekuwa ukikwama mara kwa mara.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.