Warejea Rasmi Kuwavaa Township Rollers
-Obrey Chirwa aliyeumia misuli ya Paja kwenye mchezo wa Njombe Mji amerejea rasmi na yuko tayari kuwakabili Townships Rollers ya Botswana hapo kesho.
-Papy Tshishimbi aliumia kwenye mchezo wa Ndanda na alishidwa kuelendelea na mchezo kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya naye uanaambiwa yupo fit asiliamia mia kwa sasa.
-Andrew Vicent Dante Beki kisiki naye amerejea Dante amekosa mechi Tano za ligi kuu baada ya kuumia kwenye mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ihefu Fc ya Mbeya na sasa kwa mjibu wa daktari wa klabu ya Yanga amesema Dante amejiunga na kikosi tangu ijumaa iliyopita na yupo vizuri yatabaki maamuzi ya mwalimu kumtumia au laah kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Townships Rollers.
-Yohana Mkomola Kijana kinda aliumia kwenye mchezo dhidi ya wazee wa kupapasa timu ya Ruvu shooting amekosa michezo saba mpaka sasa Daktari amesema Yohana ameanza mazoezi mepesi muda wowote atakuwa fit asilimia mia.
-Thaban Kamusoko naam unaambiwa mzee wa kampa kampa tena naye yupo fit kwa asilimia 80 limebaki jukumu la mwalimu kumpa hata dakika chache kwenye mchezo wa kesho
-Donald Ngoma Baada ya tetesi mbalimbali kuibuka juu yake naye ameanza mazoezi mepesi ndani ya kikosi cha Yanga, Ngoma ambaye alikuwa nje tangu septemba mwaka jana akiuguza majeraha ya goti ameanza kujifua mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo kesho hatakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Rollers kwa sababu hajawa fit asilimia 100.
-Ambao bado kurejea kwa sasa ni Wawili tu Mshambuliaji Amis Tambwe ambaye amefanyiwa upasuaji mdogo katika goti lake na itamchukua muda kidogo kurejea uwanjani, huku Abdalah Shaibu Ninja bado anauguza majeraha ya mguu aliyoyapata kwenye kombe la mapinduzi huko Zanzibar.
-Klabu ya Yanga kesho majira ya Saa 10:00 jioni katika dimba la Taifa Dar watacheza mchezo wa mkondo wa kwanza ya klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) dhidi ya Mabingwa wa Botswana klabu ya Townships Rollers baada ya mchezo huu watarudiana wiki moja huko Botswana.
-Mshindi wa jumla kwenye mchezo huu atafuzu moja kwa moja kwenye makundi ya klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) na atapata Fedha bilioni 1.2 kwa kufuzu hatua hiyo na iwapo timu itatolewa itaenda kucheza Play off ya kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup)
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.