Ushindi Wa Stars Wamkuna Manara Amumwagia Sifa Mchezaji Huyu.


Muda mchache baada ya kutamatika kwa dakika 90 za mpambano kati Tanzania na Dr Congo, Afisa habari wa klabu ya Simba,Haji Manara amibuka na kummwagia sifa kedekede kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba, Shiza Kichuya.

Kichuya ambaye ameonekana kuwa lulu kwenye mchezo kwa kuhusika kwa asilimia kubwa katika ushindi Stars ilioupata.

Manara kupitia instagram yake ameandika.

Haji Manara:Shiza Kichuya anaendelea kuprove kuwa yy ni zaidi ya mashine uwanjani..anajituma to the maximum..asipofunga ataassist..dunia pia imeshuhudia muunganiko murua zaid baina @kichuya_ capatenho @samagoal77 na New @msuva27 ..Heko Taifa Stars na hongera watanzania wote 🇹🇿🇹🇿 @tanfootball 🙏👏
Haikuishia hapo, Manara ameendelea kuonyesha ubora wa mchezaji huyo kwa kuwakumbusha takwimu mbalimbali za michezo aliyofanya vizuri.

Haji Manara: Sitaki kumfananisha na La Pulga..kwangu ni dhambi kuu isiyohitaji msamaha hata wa Shetani..ila kwa vwango vya kibongo bongo huyu ndio La Pulga wetu..kitu kinachowafananisha ni kufunga na kuassist..halaf anafunga ktk game kubwa..nadhani tunaelewana vzuri hapo hususan wale wabishi wabishi..nakuletea kdogo tu goli za Tanzanian la pulga kichuya na miassist yake kama mvua @kichuya_ 👏👏🙌
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.