Lwandamina ataja mchawi wa ushindi kimataifa
Baada ya klabu ya Yanga kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina, amesema kuwa hawatafanya makosa tena kwenye uwanja wa nyumbani katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Lwandamina amesema kuwa baada ya kutupwa nje katika michuano hiyo na kuangukia katika ile ya Kombe la Shirikisho Afrika, watahakikisha wanafanya vizuri katika mechi zote watakazocheza nyumbani.
Alisema kushindwa kwao kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani, ndiyo kumesababisha waondolewe katika michuano hiyo hivyo hawataki tena jambo hilo litokee.
“Tumejifunza na sasa tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi za nyumbani, kama tungefanya vizuri katika mchezo wetu wa kwanza tungesonga mbele.
“Vijana wangu walijitahidi sana kupambana katika mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Township Rollers lakini tulishindwa kupata ushindi, kwa hiyo katika mechi zetu zijazo ni lazima tufanye vizuri nyumbani,” alisema Lwandamina.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.