Baada Ya Kupata Ajali Sasa Kurejea Dimbani Wiki Ijayo..



Beki wa Simba, Salim Mbonde, anatarajia kujumuika kikosini na wenzake kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya mazoezi.

Beki huyo alikua nje ya uwanja kufuatia kuwa majeruhi, baada ya kupata ajali ya pikipiki na kupekelea kuumia jicho lake moja.

Inaelezwa Mbonde tayari amefumuliwa nyuzi ambazo alishonwa kwenye jicho, na kwa maendeleo ya sasa ya hali yake, Jumatatu atarejea kuungana na wenzake kikosini.

Kurejea kwa Mbonde kikosini kutampa kazi ya ziada kumshawishi Kocha Mfaransa, Pierre Lechntre, ili aweze kumpanga kwenye kikosi cha kwanza, na hii ni kutokana na kukosekana Dimbani kwa muda mrefu.
Join us on WHATSAPP 
 Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.