Kikosi cha Simba chapigwa 'stop'
Kikosi cha wachezaji soka nchini Tanzania, Simba kimepewa mapumziko mafupi ya kutofanya mazoezi ya aina yeyote kuanzia leo kwa lengo la kuweka viungo vyao sawa baada ya kurudi nchi kutokea katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Hayo
yameelezwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo asubuhi ya
leo kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuweza kuwapa muda mzuri wachezaji
wao wa kupumzika ili waweze kujiweka sawa katika kujiandaa na michezo
inayofuata kwenye ligi kuu Tanzania Bara inayoendelea kurindima katika
baadhi ya viwanja.
"Kikosi cha Simba kimepewa mapumziko mafupi ambapo kitaanza tena mazoezi Jumamosi kujiandaa na michezo inayofuata kwenye ligi kuu Tanzania Bara", imesema taarifa hiyo.
Simba kwa sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na alama 46 sawa na watani wao wa Jadi Yanga zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa pamoja na idadi ya michezo Yanga ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.