Kichuya: Miguu Inaniwasha
Simba kwa sasa inawaza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu tu, hiyo ni kwa kuwa ikishindwa kufanya hivyo basi michuano ya kimataifa itabaki stori.
Tegemeo pekee la Simba ni ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara maarufu kwa jina la VPL pekee, kwa kuwa tayari imetolewa katika Kombe la FA na Kombe la Shirikisho Afrika.
Kuelekea kwenye mechi 10 za mwisho wa msimu huu wa 2017/18, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya amefunguka kuwa sasa akili yake yote anaielekeza katika ligi kuu na huko ndipo atawasha moto.
Kichuya alionyesha uwezo wa juu alipokuwa akiichezea timu ya taifa, Taifa Stars ilipopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Jumanne ya Machi 27, mwaka huu.
Katika mchezo huo Kichuya alitoa pasi ya mwisho katika bao la kwanza lililofungwa na Mbwana Samatta kisha akafunga la pili kwa shuti kali la nje ya eneo la 18.
Baada ya mchezo huo, Kichuya alisema kiwango alichokionyesha akiwa Taifa Stars sasa anakihamishia kwenye ligi kuu kwa ajili ya kuisaidia Simba kubeba ubingwa.
Ikumbukwe kuwa mchezo ujao wa VPL wa Simba itakipiga dhidi ya Njombe Mji, Jumanne ijayo Aprili 3.
Katika kuonyesha mbwembwe zaidi, Kichuya alisema eti miguu inamuwasha kufanya kweli katika VPL katika michezo ijayo.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.