Mzee Akilimali kuhusu Rostand
Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, amefunguka kuwa kuna sababu kubwa ya benchi la ufundi la timu hiyo kumtumia zaidi mlinda mlango Ramadhani Kabwili badala ya Youthe Rostand kwa kuwa amekuwa akifanya makosa ya kizembe yanayojirudia kila wakati.
Mzee Akilimali alisema kuwa haoni sababu ya benchi la ufundi la klabu hiyo ya Wanajangwani kuendelea kumtumia kipa huyo katika mechi zake kwa kuwa amekuwa akigharimu timu mara kadhaa jambo ambalo linawapa wakati mgumu.
"Kiukweli msimu huu hatujapata mbadala wa makipa wetu walioondoka Yanga kama Deogratius Munishi 'Dida', Ally Mustapha 'Barthez' ambao walikuwa bora zaidi ya huyu kipa wa kigeni ambaye tupo naye hivi sasa, amekuwa akifanya uzembe mara nyingi na kuigharimu timu.
"Nadhani kuna haja ya benchi la ufundi kumuangalia yule mtoto Kabwili aliyetoka Serengeti Boys kuliko kuendelea kumtumia yule, sijui yule kipa mwingine (Beno Kakolanya) nasikia kwamba ana matatizo na uongozi, hayo siwezi kuingilia lakini huyu mgeni hatufai kwa kweli," alisema Mzee Akilimali.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.