MAKALA: HUYU NDIYE EMMANUEL MARTIN HASWAAA



Ni mmoja wa viungo washambuliaji vijana wenye uwezo mzuri wa kutengeneza magoli na kufunga. Tatizo kubwa kwa kijana huyu ni kudumu katika mwendelezo wa ubora wake uwanjani ( consistency). Angefanikiwa katika hilo angesimama kama msaada mkubwa kwa klabu yake na timu ya taifa.

Amekuwa akipanda na kushuka katika ubora wake licha ya kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza cha mzambia George Lwandamina.

Zipo sababu nyingi zinazopelekea hili kimbinu na kiufundi.

Moja, Yanga msimu huu imekuwa na tatizo kubwa la majeruhi ambao kwa namna moja ama nyingine wanaiathiri timu hiyo kimfumo na kiufundi. Kimfumo kwa maana ya tactical patterns kubadilika mara kwa mara kulingana na wachezaji waliopo katika idara husika. Hali hii pia huwaathiri wachezaji kama Emanuel Martin hususani kwenye playing partnership ambayo ina athari kubwa kwenye masuala ya kiufundi ( technical patterns) . Mwanzoni mwa ligi ,eneo la kati walikuwa wakicheza Tshishimbi na Kamusoko huku Martini akipewa wing ya kushoto kama kiungo mshambuliaji lakini kuumia kwa Kamusoko, Tambwe, Ngoma na wengineo kumelilazimisha benchi la ufundi la klabu hiyo kuja na plan B ya kumfanya Emanuel kiraka akibadilishana wings na Ajibu, Loth au Pius Buswita pia huja kati kama playmaker.

Pili, ni mfumo binafsi wa mchezaji husika kujiandaa kisaikolojia kwa kila mchezo ulio mbele yake. Kinadharia ukimuondoa mwalimu ambaye huicheza mechi kabla kwa maana ya analysis zake ambazo humpa ‘ game plan ‘ , pia mchezaji mwenye discipline nzuri na kipaji chake huanza kujiandaa kisaikolojia kuicheza mechi husika kabla ya kuingia uwanjani. Hili humfanya kujiandaa kwa mazoezi binafsi, kuwachunguza wapinzani wake, kujipa vipau mbele kulingana na mfumo na mahitaji ya mwalimu pia malengo ya muda mrefu katika kipaji chake. Emanuel anatakiwa ajitathimini katika mizani hii ili awe bora kila mechi nadhani kuna sehemu inalega kwa ubora wa kipaji chake.

Tatu, mechi mfululizo kwa ratiba iliyobana huwanyima fursa wachezaji kufanya mazoezi binafsi hususani ya fiziki na yale ya kiufundi kwa kufanyia kazi makosa ya uwanjani. Mfano upigaji wa faulo, utoaji wa pasi za mwisho, dribbling, passing and shooting in long range. Ratiba iliyobana humpa fursa mwalimu tu kutimiza majukumu yake na akiwataka wachezaji kwa saa chache wanazopata kupumzika kwa ajili ya kuondoa fatigue kitu ambacho kisipotazamwa huleta injuries pia timu kukosa kasi ( pace ). Huenda pia haya ni sehemu moja ya vikwazo vya fundi huyu kudumu katika ubora wake.

Samuel Samuel

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.