Kwa Rekodi Hizi Za Simba Kwa Mbao, Kiporo Hakichachi...


Klabu ya Simba sc jioni ya leo itakuwa mwenyeji wa klabu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza katika mchezo wa kukamilisha kiporo cha ligi kuu Tanzania bara.

Katika mchezo huo ambao umetazamwa na mashabiki na wapenzi wa kandanda kwa jicho la kipekee huenda ukawa na matokeo ya kushangaza endapo rekodi hizi zitavunjwa.

Kulingana na rekodi za timu hizi zinaonyesha kuwa Mbao wamekuwa wakipoteza wanapokutana na Simba japo kwa taabu kweli. Ukitazama katika michezo mitatu ya nyuma ambayo timu hizo zimekutana Simba imeibuka na ushindi katika michezo miwili huku Mbao wakifurukuta katika mchezo mmoja na kutoa sare.

Aidha kulingana na ubora ilionao klabu ya Simba mpaka sasa kwenye ligi na hata michuano ya kimataifa ndio unaofanya waliowengi kutabili kuwa Simba ananafasi ya kushinda mchezo huo.

Ukichukua rekodi fupi ya ligi kuu msimu huu kwa mechi tano za mwisho za Simba , Ameshinda mechi nne na kutoa sare moja.

Mechi hizo ni zile dhidi ya
Kagera Sugar  2-0
Majimaji 4-0
Ruvu Shooting 3-0
Azam FC 1-0
Mwadui FC 2-2.

Kwa upande wa Mbao FC wao katika mechi hizo wameshinda mechi 1 na kupoteza mechi 3 huku akitoa sare 1.

Mechi hizo ni zile walipofungwa na Ruvu shooting goli 2-0, na kutoa sare na  Mtibwa  0-0
Huku wakipoteza kwa Singida United gol 2-1 na kumuangukia kibonde Kagera Suga wakishinda goli 2-1 Na kukubali kipigo cha tatu dhidi ya Stand United kwa goli  1-0.

Ikumbukwe kwamba Simba ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 42 katika michezo 18 huku wakitupia kambani magoli 41 na kufungwa magoli 8 wakati wapinzani wao Mbao FC wakishikilia nafasi ya 11 wakiwa na pointi 19 katika michezo 18 na wakiwa wameshafunga magoli 17 na kufungwa magoli 20....

NB: USISAHAU KUWA MCHEZO HUU UTACHEZWA MAJIRA YA SAA 16:00(4:00) JIONI UWANJA WA UHURU...
Kwa takwimu hizi fupi je unahisi Mbao atatoka? .....Yaani kiporo Kitachach??
 Ndondoaha Comment(Maoni) uako hapo chini...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.