Kocha Kagera Sugar Azidisha Matumaini Ligi Kuu Msimu Huu...


Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema bado hajakata tamaa licha ya timu yake kuwa na mwendo wa kusuasua kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara huku akiamini timu yake itafanya vizuri. 
Kocha Maxim e ameyasema hayo muda mchache baada ya sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kupata pointi moja.
“Wote tuna macho tunaona mchezo, lakini haihusiani na matokeo, sisi kinachotuhukumu ni matokeo lakini bado sijakata tamaa bado nawapa moyo vijana wangu naamini tutafanya vizuri.”
“Mechi ilikuwa nzuri vijana wamepambana kadiri ya uwezo wao wamepata goli nao wamesawazisha mchezo umemalizika kwa sare tumepata pointi moja sio mbaya.”
Sare hiyo imeifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 14 ikiwa katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi. 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.