Azam Fc Yaanza Maandalizi Kuwakabili Singida United.

Timu ya soka ya Azam, baada ya kufuzu Robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup ASFC, imesema sasa imeelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida United ambao watacheza nao wikendi Ijayo. 
Afisa Habari wa Klabu ya Azam, Jaffary Idd Maganga amesema kuwa wanatarajia upinzani mkubwa licha ya kuwa watakuwa nyumbani. 
 "Mchezo huo unahitaji maandalizi na tutaanza maandalizi Jumatatu kwa ajili ya kuhakikisha tumejipanga vizuri na tunacheza ili kupata matoke, mchezo wa mpira hauna siri usipokuwa na maandalizi kila mtu anaona na ukiwa na maandalizi mazuri kila mtu uwanjani anaona,"
"Mwalimu atachukua nafasi ya kuweza kukaa na wachezaji tena kwa ajili ya mchezo huo, sio mchezo mwepesi ni mchezo mgumu Singida United ni timu nzuri ambayo imepanda ligi kuu na imeonesha dhamira ya kupambana katika mechi zao", amesema Maganga. 
Nafasi ya nne
Azam FC ambao kati ya michezo mitano ya hivi karibuni wamefanikiwa kupata ushindi katika mchezo mmoja kutoka sare michezo miwili na kupoteza miwili, wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi Kuu soka Tanzania Bara wakiwa na alama 35. 
Wakati wapinzani wao Singida United wakiwa karibu yao na alama 34 katika nafasi ya nne hivyo ushindi wowote utawahakikishia kuwaacha wenzao kwa tofauti ya pointi. 
Michezo mitano ya Azam iliyopita 
FT: Lipuli 0 -0 Azam 
FT: Kagera Sugar 1 - 1 Azam 
FT: Simba 1- 0 Azam 
FT: Azam 3 - 1 Ndanda 
FT: Azam 1 -2 Yanga

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.