Yanga yatua Kigali kamili gado



Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Kigali nchini Rwanda tayari kwa mchezo wao wa kesho Jumatano dhidi ya Rayon Sport ya hapa.


Yanga imewasili asubuhi hii ikitokea Tanzania tayari kukutana na Rayon Sport ikiwa ni mchezo wa mwisho wa kombe la shirikisho hatua ya makundi utakaopigwa kesho.


Baada ya kufika Yanga ililazimika kusubiri kwa dakika 45 kutoka uwanja wa ndege kufuatia kuchelewa kwa usafiri uliotakiwa kuwachukua.


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hali ya uchovu kidogo iliwakumba wachezaji wake kwa kukaa uwanjani hapo, lakini haitawaathiri.


Zahera amesema katika msafara wake wamewaacha wachezaji kadhaa kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo Juma Abdul (majeruhi), Mwinyi Haj i(baba yake mgonjwa), Said Makapu (amefiwa na mama yake), Pappy Tshishimbi (matatizo binafsi)


Aidha Zahera amesema kuelekea mchezo huo wa kesho hawana cha kupoteza ambapo presha kubwa itakuwa kwa wapinzani wao.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.