Kelvin John ‘Mbappe’ kazitosa Simba, Yanga malengo yake ‘yakiutu-uzima’
Kelvin John ‘Mbappe’ amekuwa gumzo sana kwenye timu ya taifa ya vijana wa U17 Serengeti Boys mshambuliaji anaevaa jezi namba 10.
Inawezekana umemuona lakini hufahamu historia yake hadi kufika Serengeti Boys.
Jina
Kelvin Pius John mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’, nina umri wa miaka 16 nipo kidato cha pili.
Ni mtoto wa ngapi kwa mzee Pius John?
Tupo wawili, kwa upande wa mama nipo pekeangu lakini kwa baba tupo wawili, mimi ndio mtoto wa kwanza.
Form Two mwaka huu wana fanya mtihani wa taifa, anajigawa vipi shule na mpira?
Nikiwa kambini kabla ya mashindano, kuna program naifanya kupitia laptop yangu. Natumiwa material ya shule na home work au vipindi vilivyoendelea darasani wakati mimi sipo mwalimu ananitumia kupitia email yangu nafanyia kazi. Natumiwa mitihani pia nafanya halafu namtumia tena mwalimu.
Elimu ni kitu kikubwa, mpira una mwisho naweza kufika umri ambao huwezi tena kucheza mpira lakini ukiwa na elimu unaweza kufungua kampuni na kujiendeleza.
Wengi wamemuona Kelvin John akiwa Serengeti Boys, Kelvin ameanzia wapi?
Nimezaliwa mkoani Morogoro na nimeanza kucheza mpira hapohapo Moro kwenye kituo kinachoitwa Elimu Sports Academy baada ya hapo nikaenda mashindano ya UMITASHUMTA mwaka jana nikachaguliwa na kituo kinaitwa Football House Academy cha Mwanza. Nimekaa hapo kwa mwaka mmoja sasa na ndio mafanikio yangu yameanza kuonekana.
Hakuna kabisa historia ya mwanasoka kwenye familia ya Kelvin
Kwetu hakuna mchezaji hata mmoja ni mimi pekeangu ndio wa kwanza. Baba yangu hakuwa mchezaji, katika familia yetu hakuna mtu ambaye aliwahi kuwa mchezaji.
Kipaji chake kilijulikana vipi?
Nikiwa mdogo katika shule ya msingi Mwele nilianza kucheza mpira katika ngazi ya shule nikapata fursa ya kuchaguliwa ngazi ya mkoa mwaka 2016 katika mashindano ya UMITASHUMTA ndipo hapo nikaanza kuonesha uwezo wa juu babaangu akaanza kuniruhusu nicheze mpira na safari ya mafanikio ikaanzia hapo.
Baba Kelvin ana mchango gani hadi alipofikia mwanae?
Baba yangu ana mchango mkubwa hadi hapa nilipofika kwa sababu amekuwa ananipa support muda mwingine nakosa nauli ya kwenda mazoezini lakini anafanya jitihada hata ikibidi kukopa ili niende mazoezini. Amenipa hamasa kubwa ili nicheze mpira na kufanikiwa.
Kitu kikubwa anachoniambiaga ni kufanya vema katika mpira, nizingatie nidhamu kwa sababu nidhamu ndio msingi wa maisha yangu. Kabla ya sijaja katika mashindano haya nilimwahidi baba nitamfanyia surprise kubwa katika mashindano haya na mwenyewe anaona.
Tangu niingie kambini sijawasiliana nae kwa sababu haturuhusiwi kutumia simu tukiwa kambini tukiwa tunajiandaa na mashindano. wakati nakuja kambini mara ya mwisho niliongea nae na aliniombea dua akanitakia kila la heri katika mashindano haya.
Ninapokuwa uwanjani sifikirii kuhusu mzazi, nafikiria mechi, nifanye nini ili timu yangu ipate ushindi dhidi ya timu pinzani.
Malengo ya Kelvin
Malengo yangu ni makubwa. Kitu cha kwanza ni kumsikiliza mwalimu nini anasema, walinu wangu wanaonifundisha wote wazuri. Jukumu langu kama striker ni kufunga ni lazima nifundishwe mazoezini jinsi ya kufunga ili kwenye mechi nisipate wakati mgumu katika kufunga. Kazi yangu ni kufunga nawaahidi watanzania nitafunga sana.
Ndoto yangu ni kucheza nje na kuwa mchezaji mkubwa duniani ili niwe mwakilishi mzuri katika taifa langu Tanzania.
Vilabu vinapigana vikumbo kumgombea
Mwalimu wangu ambaye nipo naye hapa anasumbuliwa sana na timu nyingi kila akiwaambia wasubiri hadi mashindano yaishe ili waongee lakini bado wanazidi kumsumbua wanampigia simu kutanga kuongea nae kuhusu mimi.
Wakati mwingine inabidj nikae sana ndani, watu wanakuja kambini wanahitaji mazungumzo na mimi lakini siwezi kuzungumza hadi mashindano yaishe ndio nitazungumza pia mimi sio muongeaji nina mtu ambaye ananisimamia ndio watazungumza naye.
Mimi bado sijafikia umri wa kusaini mkataba na timu yoyote bado sina uamuzi wa kuchagua timu lakini timu yoyote itakayokuja siwezi kusaini mkataba kwa sababu umri wangu bado mdogo.
Kazitema Simba na Yanga
Ndoto yangu ni kucheza nje sio katika soka la Tanzania kwa sababu mpira wa Tanzania ukicheza katika timu kubwa Simba na Yanga su timu yoyote ndio mpira wako unaishia hapo lakini ukicheza nje ya mipaka ya Tanzania kiwango chako kitakuwa kama kakaetu Mbwana Samatta alivyofanikiwa.
Samatta ndio role model
Mbwana Samatta ndo role model wangu, hadi sasa hivi naiga vitu vingi kutoka kwake akiwa uwanjani jinsi anavyoisaidia timu yake ya KRC Genk na anavyoisaidia timu ya taifa. Na mimi nakikisha nitafanya vizuri nikiwa na timu yangu ya taifa ya vina na kufikia malengo tuliyojiwekea ya kufika World Cup ya vijana mashindano yatakayofanyika Peru.
Tunawaahidi watanzania tutaifikisha timu hii World Cup
Source: Shaffihdauda.co.tz
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.