Ujumbe Mzito Wa Salum Mkemi Kwa Uongozi Wa Yanga Baada Ya Kujiuzulu..
Salum Mkemi Yanga. |
Mkemi ameandika
'Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi Kwa Hakika Tumepata Aibu Kubwa Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele"
"Pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza"
" Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club "YANGA " kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018"
"Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane. Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu SALUM MKEMI"
Hayo ameyasema Salum Mkemi jioni ya leo baada ya klabu ya Yanga kuendelea kuwa na matokeo mabaya. Hii si mara ya kwanza kwa Mkemi kujiuzulu alishawahi kuandika barua kwa katibu wa klabu ya Yanga Kujiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya klabu ya Yanga ila alikuja akabadirisha msimamo huo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.