NGOMA KUONDOKA USIKU WA LEO KUELEKEA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU



Aliyekuwa mchezaji wa Yanga SC kutoka nchini Zimbabwe na sasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Azam Donald Ngoma anatarajia kuondoka usiku wa leo akielekea nchini Afrika kusini kwaajili ya matibabu.

Awali Ngoma kabla ya kujiunga na Klabu ya Azam hakuweza kuichezea Timu yake ya Zamani (Yanga) kwa kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Msemaji wa Klabu ya Azam FC Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa mchezaji huyo ataondoka usiku wa leo na kuelekea nchini Afrika kusini katika mji wa Cape Town ilipo hospital ambayo Wachezaji wa Klabu hiyo wanatibiwa katika Hospital hiyo. .
"kama ilivyo awali nilisema kuwa mchezaji wetu Donald Ngoma aliyetoka Klabu ya Yanga tumemsaini kuja kuitumikia Klabu yetu ya Azam FC ni majeruhi hivyo sisi kama Azam tunampeleka mchezaji huyu katika hospital ambayo wachezaji wetu wanatibiwa iliyopo mji wa Cape Town nchini Afrika kusini, na katika safari hii Ngoma ataambatana na Dactari wetu Dkt. Mwanandi Mwankemwa na baada ya vipimo hivyo majibu yakija kuwa Ngoma anatatizo lolote tutaghalamia matibabu yake mpaka atakapo kaa sawa ili msimu ujao ukianza awe fiti "amesema Maganga

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.