Mfaransa Mwingine Atajwa Kutua Simba
Inaelezwa kuwa mabosi wa klabu ya Simba wameanza mazungumzo na Mfaransa mwingine atakayerithi kiti cha Pierre Lechantre ambaye amenyimwa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Taarifa za ndani zinasema Hubert Velud ni jina la kocha ambaye anahusishwa kuja kuinoa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Velud amewahi kuzinoa klabu kubwa barani Afrika ikiwemo Etoile du Sahel, ES Setif, TP Mazembe pia timu ya taifa ya Togo.
Mfaransa huyo anaweza kuja nchini kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenzake ambaye mkataba wake umeshamalizika baada ya kusaini miezi 6 inayomalizika siku chache zilizosalia.
Na taarifa zilizopo kwa wekendu hao wa Msimbazi ni kuwa tayari wameshaachana na Lechantre kutokana na kutorodhishwa na kiwango chake ndani ya timu na sasa wameanza mazungumzo na makocha wengine ikiwemo Velud anayehusishwa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.