Yanga yaondoka nchini kuelekea Kenya kwenye SportPesa Super Cup, Ajibu hajaonekana kocha afunguka (+video)


Kikosi cha klabu ya  Yanga leo Alhamisi majira ya saa 10:45 jioni kimeondoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup kupitia shirika la ndege la Kenya Airways.

Kikosi hicho ambacho baadhi ya nyota wake hawajaonekana uwanjani hapo akiwemo Ibrahim Ajib kimeondoka kikiwa na matumaini ya kufanya vizuri zaidi ingawaje kocha wa klabu hiyo, Zahera Mwinyi amedai kuwa michuano hiyo ni kama maandalizi kwao ya msimu mpya unao kuja.
Hata hivyo, viongozi wote wa Yanga wamekataa kuzungumzia kukosekana kwa Ajib kwenye kikosi hicho kilichoondoka jioni ya leo kuelekea Kenya.



No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.