Kelele za Manara zafika Bungeni



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola leo bungeni ameweka wazi kwamba japokuwa uchafuzi wa mazingira ni pamoja na upigaji wa kelele kwa mujibu wa sheria lakini kelele za ushabiki zinaruhusiwa kwa mujibu wa muongozo.

Mhe. Lugola amefunguka hayo leo Mei 14 bungeni ambapo amesema karibuni kulizuka kelele ambazo yeye aliulizwa sheria ya mazingira inasema nini kuhusiana na kelele baada ya watu kushangilia tamko la Msemaji wa Klabu ya Mabingwa Tanzania Bara Simba, Haji Manara kuhusu mchezo wa Simba na Yanga ili kuisaidia timu hiyo kimapato.

"Juzi Haji Manara wakati anatangaza mechi kati ya Simba na Yanga ili waisaidie yanga mapato kelele zilikuwa nyingi sana. Nikaulizwa haya makelele kwa mujibu wa mazingira yanamahusiano gani? Nikasema kwa mujibu wa kifungu cha 106 haya makelele yanazuiwa lakini yale yakushabikia matamko kama ya Haji Manara yanaruhusiwa kwa mujibu wa muongozo". Lugola.

Mbali na hayo Mh. Lugola amejibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Jasmine Tisekwa kuhusu hatua gani serikali imechukuwa katika kuzuia ujenzi holela unaofanyika katika vyanzo vya maji huko katika milima ya Pangawe, na Kigurunyembe.

Mh. Lugola amesema kuwa tayari amekwishatoa maagizo katika maeneo hayo ya kwamba mpango mkakati wa kushughulikia uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kulinda vyazo vya maji

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.