KAHEZA AIOMBA RADHI SIMBA BAADA YA KUFANYA HILI.


Mshambuliaji mpya wa Simba, Marcel Kaheza amewaomba radhi mabingwa hao kwa kuwafunga akiwa na timu yake ya zamani ya Majimaji katika mchezo wa kufungia pazia la ligi jana.

Kaheza alifunga bao hilo dakika ya sita katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao moja baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Simba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kaheza aliomba radhi kwa Simba akisema alikuwa akitimiza majukumu ya kazi na waajiri wake wa zamani Majimaji.

"Naombeni mnisamehe mashabiki wa Simba, mechi haikuwa na umuhimu mkubwa kwenu kwakua mshachukua ubingwa, nawapenda sana," alisema Kaheza.

Mshambuliaji huyo alikulia katika kikosi cha vijana cha Simba miaka kadhaa iliyopata lakini alikosa nafasi kutokana na kukutana na wachezaji waliomzidi uwezo.

Msimu huu umekuwa mzuri kwa Kaheza baada ya kufunga mabao 14 sawa na John Bocco huku timu yake ikishuka daraja.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.