Jonas Mkude mchezaji pekee aliyedumu Simba tangu ilipochukua VPL kwa mara ya mwisho.

Kiungo wa kati wa Simba, Jonas Mkude amesema haoni sababu ya kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wapya wa ligi kwakua anapata kila kitu kwa Wekundu hao.

Mkude ni mmoja wa wachezaji watatu wa Simba waliokuwepo kwenye kikosi cha mwisho kilichochukua ubingwa mara ya mwisho 2012/13.

Mbali na Mkude wachezaji wengine waliokuwepo kwenye kikosi kilicho chukua ubingwa ni Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.

Mkude ambaye anaamiwa na kocha Mfaransa Pierre Lechantre amesema amepitia changamoto nyingi ndani ya Simba lakini amevumilia na sasa kila kitu kinaenda vizuri.

Kiungo huyo amesisitiza kuwa mpira ndio kazi yake hivyo anafahamu kuna siku ataondoka ndani ya Wekundu hao kutafuta maisha sehemu nyingine.

"Mimi ni mmoja wa wachezaji waliodumu na Simba muda mrefu na nimepitia changamoto nyingi lakini nimevumilia mpaka leo nipo hapa.

"Ila mpira ni kazi yangu kwahiyo kila kitu kinawezekana sijui nini kitatokea huko mbeleni ila nafurahi kuwa sehemu ya wachezaji waliochukua ubingwa msimu huu," alisema Mkude.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.