Habari Na Tetesi Zote za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara VPL Wiki Hii. {Djuma Kubeba Mikoba Ya Lechantre}

Makocha wa Simba (Pierre Lechantre na Masoud Djuma)

Tuanze na hii ya klabu ya Simba kuinasa saini ya straika wa klabu ya Majimaji, Marcel Kaheza.

Taarifa zinaeleza kuwa wekundu wa Msimbazi tayari wamefanikiwa kuinasa saina ya mpachika mabao wa klabu ya Majimaji Marcel Kaheza licha yakiwa hakuna taarifa maalumu kutoka Simba wala Majimaji ila kwa mujibu wa mchezaji mwenyewe amehakikishia umma kuwa yeye ni mchezaji mpya wa Simba kwa msimu ujao.

Nyingine ni hii, Simba yaypiku Yanga kwa Adam Salamba.

Klabu ya Simba imetangaza kumsajili kiungo Mshmbuliaji Wa Lipuli fc, Adam Salamba kwa kandarasi ya miaka mitatu kuanzia msimu ujao.

Ujio huo wa Salamba Simba umeviweka mashakani vibarua na hatima za nyota wakongwe wa Simba kama Laudit Mavugo na Juma Luizio huku Mohamed Ibrahim "Mo" akielezwa kuwa mashakani kuendelea kukitumikia kikosi hicho baada ya kutaka dau la Shillingi Millioni 70 na hii ni kwa mujibu wa gazeti la Championi.

Pluijm apanga kuibomoa Yanga.

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Mholanzi Hans Van Pluijm ameweka wazi nia yake ya kuwanyakuwa mabeki wa klabu hiyo, Kelvin Yondani na Ju.a Abdul.

Wawili hao ambao tayari hapo awali walifanya kazi na Pluijm kwa mafanikio wametajwa kuondoka na kuungana na nyota mwingine wa Yanga Ambaye tayari amekwisha kusaini mkataba na Azam ambaye ni Donald Ngoma.
Donald Ngoma akisaini mkataba Azam fc.


Mrisho Ngassa Kurejea Yanga.

Baada ya misimu kadhaa ya kupotea kwenye ululimwengu wa soka hatimae mshambuliaji wa Zamani wa klabu ya Yanga, Mrisho Ngassa ametajwa kurejea kunako klabu hiyo akitokea Ndanda Fc ambako amekuwa na kiwango kizuri tangu alipojiuna na klabu hiyo akitokea Mbeya city.

Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa  wanajangwani hao wanatarajiwa kufungua dirisha kwa kukamilisha usajili wa straika huyo ambaye aliwika vyema akiitumikia klabu hiyoenzi za miaka ya nyuma.


Pierre Lechantre Ataka Mshahara Mkubwa.

Baada ya kuiwezesha Simba kutwaa Ubingwa, kocha mkuu wa klabu hiyo Pierre Lechantre amesema anataka kuongezewa mshahara au la anaweza kuondoka klabuni humo (Gazeti La Dimba Limeripoti)

Kocha huyo aliyejiunga na Simba kwa mkataba wa miezi sita akichukua nafasi ya Mcameroon, Joseph Omog kwa sasa yupo huru na anahitaji Mshahara Mnono  ili kuendelea kuinoa Simba.

Djumaa Kuwa Kocha Mkuu Simba.

Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djumaa amesema anaweza kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo endapo Mfaransa Pierre Lechantre ataondoka klabuni humo.

Djuma amesema "naweza kuwa kocha  mkuu kwa sababu ninajiamini kulingana na uwezo wa kuongoza timu".

Juma Mahadhi Atakiwa na klbu yake ya Zamani.

Baada ya kurejea ligi kuu klabu ya Coastal Union imesema ikotayari kumrejesha winga wake wa zamani, Juma Mahadhi ambaye hajawa na msimu mzuri na klabu yake ya sasa ya Yanga sc.

Mkataba wa unatarajiwa kumalizika mwezi ujao na huenda akatumia nafasi hiyo kujiunga na wagosi wa kaya kwa msimubjuao.

Wachezaji 11 Yanga mikataba Yao Imekwisha.

Imeripotiwa kuwa wachezaji 11 wa kikosi cha Yanga mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu hivyo dirisha kufunguliwa wakiwa ni wachezaji huru.

Wachezaji hao ni pamoja na Nadir Haroub, Hassan Kessy, Vincente Andrew, Obrey Chirwa na Kelvin Yondani.

Wengine ni, Beno Kakolanya, Emmanuel Martin, Geofrey Mwashiuya, Juma Abdul, Juma Mahadhi na Said Juma.

Kwa Tetesi Na Dondoo Mbalimbali za usajili VPL endlea kuwa nasi.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.