Usajili: Kocha Julio Kutua Yanga Kutwaa Mikoba Ya Lwandamina.
Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema yupo tayari kuchukua mikoba ya Mzambia, George Lwandamina pale Jangwani endapo watakubaliana.
Akiongea na E Sports ya EFM Julio amesema kuwa anaamini anaweza kuinoa Yanga kutokana na uzoefu wake wa kufundisha soka hapa nchini pamoja na nje ya nchi.
"Niliwahi kupata nafasi Yanga ili niwe Kocha, lakini kuna baadhi ya watu waliokuwa hawana nia njema wakati Abbas Tarimba akiwa kiongozi waliniharibia mipango" Alisema Julio.
Julio anaamini anaweza kuifundisha Yanga kutokana na uzoefu alionao ndani ya soka la Tanzania sababu akieleza ameshafundisha baadhi ya timu hapa nchini.
"Nipo tayari kufundisha kama watakubaliana namimi, nina uzoefu wa kutosha katika kazi hii" amesema.
Ikumbukwe kuwa Yanga kwasasa iko chini ya aliyekuwa kocha wa Viungo wa klabu hiyo aliyeshika mikoba hiyo kwa muda baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo.George Lwandamina.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.