Taarifa Kutoka Simba Kuhusu Hali Ya Emmanuel Okwi Baada Ya Majeraha Aliyoyapata Kwenye Machi Dhidi Ya Mbao Fc.
Mshambuliaji wa kimataifa Emmanuel Okwi anaendelea vizuri kutoka kwenye majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mbao FC.
Daktari wa timu hiyo Yassi Gembe kuhusianana na hali ya Okwi amesema, 'Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii'.
Kikosi cha Simba kesho kutwa tarehe 2.3.2018 kitavaana na timu ya Stand United.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.