Msimamo Wa Ligi Kuu Tanzania Baada ya Mechi Ya Yanga Na Ndanda Fc.

Mchezo wa kukamilisha mzunguuko wa 19 ligi kuu ya Vodacom umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 hivyo kupunguza tofauti ya alama dhidi ya vinara Simba kubaki tano.

Yanga imefikisha alama 40 na kubakia nafasi ya pili huku Simba ikiwa kileleni na alama 45.



Azam FC iko nafasi ya tatu na alama 35 na Singida United iko nafasi ya nne na alama 34 kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo juu.

Michezo mitano ijayo ya Yanga, mmoja utachezwa mkoani dhidi ya Mtibwa Sugar huku mingine minne ikipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Baada ya kusafiri mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kucheza na timu za Kagera Sugar, Stand United, Simba na Singida United.

Kwa upande wa Simba, Ijumaa itashuka uwanja wa Taifa kuivaa Stand United, kisha itakwenda mikoani kuzivaa Mtibwa Sugar na Njombe Mji halafu itarejea Dar kuzivaa Yanga, Mbeya City na Prisons.

Ligi bado ni mbichi sana na kwa anayejitangazia ubingwa wakati huu atakuwa anajidanganya.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.