Hawa Hapa Waamuzi Watakaochezesha Mecha Kati Ya Yanga Na Township Rollers
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya
Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17, 2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.
Simba v El Masry.
Wakati huo huo CAF imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7, 2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.