Chirwa Akanusha Kutaka Mamilioni Ya Pesa Ili Kusaini Mkataba Mpya Yanga, Soma Zaidi Hapa>>>>


Stamraika wa klabu ya Yanga, Obrey Chirwa amekanusha taarifa za yeye kuhitaji mamilion ya pesa ili kusaini mktaba mpya.

Chirwa aliyekuwa akihusishwa na kuhitaji  shillingi million 150 ilikuweza kusaini kandarasi mpya kunako mitaa ya Jangwani amekanusha taarifa hizo na kuongeza kuwa amechukizwa na wanavyomzushia na anadhani wanahitaji kumgombanisha.

"Sijawahi kusema  popote nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia,nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.
Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi,mimi ni mchezaji wa Yanga". - OBREY CHIRWA. 

Chirwa ameshindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya majimaji . 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.