Lipuli Waichalaza Ndanda FC, Wathibitisha Ukweli Wa Sanga..
Wanapaluhengo timu ya soka ya Lipuli wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Samora mjini Iringa wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wanakuchele Ndanda FC.
Mabao yoe ya Lipuli katika mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji matata Adam Salamba wakati bao pekee na la kufutia machozi la Ndanda FC limefungwa na Nassoro Kapama katika dakika ya 21.
Matokeo hayo yanawafanya Lipuli kufikisha alama 23 na kuchumpa kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya tisa hadi nafasi ya saba wakati Ndanda wakisaliwa na alama 18 na kuendelea kukalia nafasi ya 13
Baada ya matokeo hayo tunaweza kusem kuwa wachezaji wa Lipuli hawajamuangusha msemaji wao, Clement Sanga kwani juzi alitoa ahadi ya kuiadhabu Ndanda kwa idadi sawa na magoli yaliyofungwa jana na Lipuli.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.