Wachezaji Watano (5) Majimaji Fc Wasimamishwa Kuelekea Mechi Ya Leo Dhidi Ya Yanga.


Kocha wa Maji Maji, Habib Kondo amewataja wachezaji waliosimamishwa ni Andrew Ntala, Sadik Galacha, Paul Maona, Alex Kondo na Six Mwasegaga.

Kondo alisema kwamba wachezaji wote hao wamesimamishwa kwa kosa la kugoma kufanya mazoezi, huku pia wakiwachochea wachezaji wengine kufanya hivyo.

Lakini taarifa zinasema wachezaji hao waligoma ili kushinikiza kulipwa stahiki zao mbalimbali, ikiwemo malimbikizo ya mishahara, fedha za usajili na posho.

Kondo amesema kuondoka kwa watano kunafanya idadi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza walioondoka Maji Maji kufika saba, baada ya kuondoka kwa Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Kenneddy Kipepe.

Lakini Kondo amesema kwamba tayari amechukua wachezaji kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kuziba nafasi hizo na anaamini watafanya vizuri.

“Ukweli ni kwamba wachezaji walioondoka walikuwa wa kikosi cha kwanza kwa hiyo ni pigo katika timu, lakini kwa kuwa tupo vitani tutaingia kupambana na hawa hawa tulionao,”alisema Kondo.
Majimaji fc watakuwa wenyeji wa Yanga leo katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la Shirikisho(ASFC). 

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.