Je Manji Atarejea Yanga Au La?
Mfanyabiashara Yusuph Manji ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga unaotarajiwa kufanyika Juni 10, jijini Dar es salaam.
Jana Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alithibitisha kualikwa kwa Mwenyekiti na Mfadhili huyo wa zamani wa Yanga
Wakati Yanga iko tayari kwa mabadiliko, utakuwa ni wakati muafaka kwa Mfanyabishara huyo mwenye mapenzi makubwa na klabu ya Yanga kurejea.
Pamoja na matatizo yaliyomkumba, inaelezwa sababu kubwa iliyopelekea ajiuzulu mwaka jana ni kupingwa kwa mpango wake kuikodisha Yanga.
Lakini tangu ajiweke kando, hali ya Yanga imekuwa 'taabani' kupelekea hata wale waliokuwa wakimpinga kujiweka kando na wengine kumuomba arejee.
Naamini mfumo mpya wa uendeshaji unaokwenda kuridhiwa na Wanachama wa Yanga unawahitaji sana akina Manji na wawekezaji wengine wenye mapenzi na klabu ya Yanga.
Mfumo huo mpya ambao tayari uko kwenye Katiba ya Yanga utawezesha wawekezaji kumiliki hisa kwa asilimia 49 wakati asilimia 51 zitaendelea kubaki kwa wanachama hivyo kuondoa malalamiko ya wanachama 'kuporwa' timu yao.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.