YANGA, SIMBA NA AZAM KUSHIRIKI KOMBE LA KAGAME

Na Joseph michael
-Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame inatazamiwa kufanyika nchini baada ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, Tff kuthibitisha kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

-Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, Wallace Karia amesema Tanzania bara itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka huu na Yanga Sc itashiriki kama bingwa wa bara wakati Simba itaingia kwakuwa wameomba iwemo hasa kwakuwa bara imekuwa mwenyeji.

-Karia amedai Azam Fc ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo hivyo wataingia kutetea taji lao, timu 16 kutoka mataifa ya Afrika mashariki na kati zitashiriki, michuano bado inadhiminiwa na Rais wa Rwanda, Poul Kagame na inaendelea kutambulika kama kombe la Kagame

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.